Image
Image

Serikali kuwarudisha nchini Watanzania waishio Yemen


Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ametangaza hatua ya Serikali ya kuwarudisha Watanzania waishio nchini Yemen, kufutia mapigano yanayoendelea nchini humo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Akizunguza na Mhe. Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman siku ya Alhamis tarehe 16 Aprili 2015, Waziri Membe amesema ni jukumu la Serikali kuhakikisha kuwa Watanzania hao ambao wengi wao ni wanafunzi, wanarejea nyumbani salama.
Awamu ya kwanza ya kurudisha Watanzania ilifanyika siku chache zilizopita chini ya uratibu wa Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Mascut, Oman. Kwenye awamu hiyo Watanzania ishirini na tano (25), walirudishwa nyumbani huku jitihada za kuandikisha wengine zikiendelea.
“Nimeruhusu matumizi ya fedha ya dharura ili kuhakikisha ndugu zetu walioko kwenye hatari na machafuko ya Yemen wanarejeshwa salama nyumbani mara moja,” alisema Mhe. Membe.
Watanzania hao ambao wengi wao hadi sasa wameshafika miji ya Sarfat na Al-Mazyouna iliyopo katika mpaka wa Oman na Yemen, walituma maombi ya dharura (distress call) kwenye Ofisi za Ubalozi kuelezea mazingira ya hatari yanayowakabili, ambapo zoezi la kuhakiki, kuadnikisha na kuwarudisha lilianza mara moja.
“Kwa maelekezo ya Mhe. Membe, awamu ya pili ya zoezi hili itaanza, ambapo Watanzania wote sitini na nne wataruhusiwa kuingia nchini Oman na kurejeshwa nyumbani mara moja” alimaliza Mhe. Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Waziri Membe yupo nchini Oman kwa ziara ya siku moja ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
16 Aprili, 2015
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment