Image
Image

Shambulizi katika chuo kikuu Garissa laua 17 na kujeruhi zaidi ya 70 mpaka sasa.



Rais uhuru kenyata wa kenya amesema amesikitishwa na magaidi walio shambulia leo hii katika chuo kikuu cha Garissa na kuua watu 17 kujeruhi zadi ya watu  70 na wengine kuteka nyara.

Amesema Huu ni wakati wa kila mtu nchini humo  kuwa macho kama mataifa mengine ili  kuendelea kukabiliana na kuwashinda maadui wanaojipenyeza nchini humo.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salam za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi la chuo kikuu cha Garissa kazkazini mashariki mwa Kenya.
Kiongozi huyo vilevile amewahakikishia wakenya kwamba serikali yake imechukua hatua za kuwapeleka maafisa wa usalama katika eneo hilo.
Amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.
Kwaupande wake waziri wa maswala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaiserry amethibitisha kuwa watu 15 wameuawa huku wengine 53 wakijeruhiwa kufuatia shambulizi la alfajiri katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya.
miongoni mwa waliokfariki ni walinzi wawili wa mlango wa chuo hicho.
Akizungumza kutoka Garissa Nkaiserry amesema kuwa oparesheni ya kuwasaka wahalifu hao itaendelea hadi mateka wote waokolewe.
Serikali ya Kenya imemtaja Mohammed Kuno kama kuwa mshukiwa mkuu aliyepanga njama za shambulizi la chuo kikuu mjini Garissa.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari waziri wa usalama nchini Kenya Joseph Nkaiserry alitoa zawadi ya dola 53,000 kwa mtu yeyote atakayemkamata mshukiwa huyo ama kutoa habari zake.
Kuno anajulikana kama 'Gama'adhere kwa jina maarufu.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment