Image
Image

Tanzania inaunga mkono tamko la mwenyekiti wa AU na SADC Mzee Robert Mugabe kuhusu machafuko ya Afrika kusini.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam, Wakati alipotoa tamko la serikali ya Tanzania kuhusu machafuko yaliyotokea wiki iliyopita nchini Afrika Kusini kwa wenyeji wa nchi hiyo kufanya mashabulizi dhidi ya wageni kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wanaoishi nchini humo.

Amesema kuna habari zimeenea kwenye mitandao mbalimbali kuwa kuna watanzania wamekufa, Ni kweli ila watanzania hao wamekufa katika matukio tofauti na vurugu hizo amesema watanzania waliokufa katika matukio hayo ni Athman China alipigwa kisu gerezani  , Rashid Mohamed aliyeuwawa kilomita 90 kwa tukio la uporaji na Ali Heshi Mohamed aliyekufa kwa  ugonjwa wa TB kutokana na maelezo ya Polisi wa nchini humo.

Waziri Membe amewataka watanzania kujiandikisha katika ubalozi wa Tanzania nchini humo ili serikali iwarejeshe nyumbani wakati serikali ya Afrika Kusini inalishughulikia suala hilo, mpaka sasa ni watanzania 23 wamejiandikisha kurejea nyumbani. Lakini watanzania wawili wamekataa kurudi nyumbani.

Amesema Tanzania inaunga mkono Tamko lililotolewa na Mwenyekiti wa SADC na AU Rais wa Zimbabwe Mzee Robert Mugabe kuhusu machafuko hayo na hatua ambazo serikali ya Afrika kusini imechukua ili kuzuia yasiendelee.
Source:FullShangwe.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments: