Zaidi ya wanafunzi 290 wa shule ya
msingi ya Nangombo katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma,wameshindwa kuhudhuria
masomo yao Darasani kwa wiki tatu kutokana na kukosa chaki za kufundishia hali
ambayo inatishia pia wanafunzi wa Darasa la saba wanaokabiliwa na mtihani wa
mwisho mwaka huu kutofanya vizuri.
Kwa zaidi ya wiki tatu mfululizo wanafunzi wakiwemo wa Darasa la Saba
katika shule hii ya msingi ya Nangombo iliyopo makao makuu ya wilaya ya Nyasa,
wameshindwa kusoma kutokana na walimu kukosa chaki za kufundishia hali ambayo
imemstajaabisha pia kamanda wa vijana-CCM katika wilaya hiyo,Bwana CASSIAN
NJOWOKA aliyetembelea shule hiyo.
Kutokana na tatizo hilo, Bwana NJOWOKA mbali ya kukabidhi BOX 25 za
chaki kwa shule hiyo, pamoja na kuahidi kuwalipa posho walimu watakaofundisha
wanafunzi wa darasa la saba hadi siku ya mitihani yao, pia anasema atajitolea
kuwapeleka Dar es salaam vijana sita kujifunza namna ya kutengeneza chaki ikiwa
ni pamoja na kununua mashine mpya ya kuzalisha chaki hizo ili ziweze kuondoa tatizo
la chaki kwa shule zote za wilaya ya Nyasa.
Kwa mujibu wa maelezo ya mwalimu mkuu wa shule hii ya msingi
Nangombo,Bwana Yasint Hyera, shule hii ipo katika himaya ya wamision wakatoriki
hivyo wametafuta eneo lingine la kujenga shule mpya huku kamanda huyo wa vijana
CCM wilaya ya Nyasa akiwataka wananchi kujitolea kufyatua tofari na yeye
atachangia BOX za marumaru pamoja na vifaa vyote vya kiwandani kwa madarasa
mawili.
0 comments:
Post a Comment