Image
Image

Wananchi walalamikia zahanati kwa kukosa vifaa tiba na miundombinu stahiki Wilayani Kishapu,Mkoani Shinyanga.



Wananchi wa Kata ya Ukenyenge Wilayani Kishapu,Mkoani   Shinyanga wanaotegemea  matibabu katika zahanati ya Negezi wamielalamikia  zahanati hiyo kwa kukosa miundo mbinu na vifaa- tiba .
Wamedai kuwa kwa muda mrefu kumekuwepo na upungufu wa wahudumu katika zahanati hiyo huku miundombinu yake ikiwa chakavu hali ina yo sababisha wagonjwa kuchelewa kupata huduma za afya , hali inayohatarisha maisha ya wagonjwa na wajawazito.
Wakazi wa Kata ya Ukenyenge wanaotegemea kupata huduma za afya katika zahanati hiyo wamesema hali hiyo inawakatisha tamaa kwani hata wananchi waliojiunga katika mpango wa huduma ya Afya ya Jamii hawapati huduma kama inavyohitajika .
Katika zahanati hiyo  baadhi ya majengo yamechakaa  na  vyoo naonekana vimedidimia na kuanguka na choo kimoja kinachotumiwa na wagonjwa pamoja na wahudumu kikiwa  na  nyufa na  kipo   hatarini kuanguka .
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Kishapu ,Bwana   MOHAMED MLEWA amekiri kuwepo kwa  matatizo hayo,  lakini amewatoa hofu wananchi kwa kusema serikali imeshaanza kushughulikia kero hiyo .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment