Image
Image

Watu waliofariki dunia katika ajali ya basi la Nganga katika eneo la Iyovi wazikwa katika kaburi moja.




Mamia ya watu wakiwa wanashuhudia ndugu na jama zao wakizikwa katika kaburi  moja  ambalo kufuatia kupata ajali iliyohusiha basi la Nganga na fuso kisha kuteketea kwa moto  Iyovi ruaha wilayani kilosa katika barabara ya Morogoro iringa.



Mamia ya wananchi wa kilosa na kilombero washiriki katika mazishi ya pamoja kwa abiria  waliokufa kwenye ajali ya basi la Nganga.


Wakazi wa wilaya za kilosa na kilombero  wamejitokeza kwa wingi katika kushuhudia  maziko  ya pamoja ya  watu kumi na tano kati ya kumi na tisa waliofariki katika ajali ya basi ya Nganga ambalo liligongana na fuso  kisha kuwaka moto katika eneo la Iyovi  na kuzikwa katika kaburi la pamoja kwenye makaburi ya Msamvu ruaha wilayani kilosa mkoani Morogoro.

Hili ndilo kaburi moja  ambalo wapendwa wetu wanahifadhiwa humu ambapo greda lina wafukia baada ya kuingizwa wote humu ndani kwenye nyumba ya milele,kufuatia kupata ajali iliyohusiha basi la N ganga na fuso kasha kuteketea kwa moto  Iyovi ruaha wilayani kilosa katika barabara ya Morogoro iringa.
Wakizungumza kwa niaba ya serikali mkuu wa wilaya ya kilosa Bw John Henjewele amesema serikali imewalazimu kufanya mazishi ya pamoja ya watu waliofariki kwenye  ajali hiyo ambao miili yao haijatambulika na kwamba serikali itaendelea na zoezi la ukaguzi wa magari amkoani  wa Morogoro ili kudhibiti ajali za mara kwa mara na kupoteza maisha ya watu huku wengine wakiachwa na vilemalema  vya maisha   ambapo mkuu wa wilaya ya kilombero Bw Lephy Gembe amewataka  wananchi  kuwa na uvumilivu katika msiba mkubwa walioupata.

Hili ndilo kaburi moja  ambalo wapendwa wetu wanahifadhiwa humu kufuatia kupata ajali iliyohusiha basi la N ganga na fuso kasha kuteketea kwa moto  Iyovi ruaha wilayani kilosa katika barabara ya Morogoro iringa.
Kwa upande wake Diwani  wa kata ya ruaha Rahel Nyangasa amesema wamepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani umekuwa ni pigo kubwa kwa wakazi wa wilaya hizo huku ndugu na waombolezaji wakisema msiba huo siwakusahaulika kwani umewastua sana ambapo naye  muinjilisti wa kanisa la kiinjili la kilutheri Issaya Chura akiomba serikali kuendelea kukabiliana na madereva wabovu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment