Image
Image

Watu wanane na wanafunzi sita wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi huku wengine wakijeruhiwa manispaa ya Kigoma.


WATU wanane wakiwemo wanafunzi sita wa shule ya msingi kibirizi Manispaa ya Kigoma wamekufa baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa kigoma Maweni,DK.FADHILI KIBAYA amesema sambamba na watu hao waliofariki pia  watu 15 wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Dk.Kibaya amewataja waliofariki kuwa ni pamoja na Yusuf Athuman, Hassan Ally, Fatuma Sley, Zamda Seif, Shukrani Yohana na Warupe Kapupa ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule hiyo ambapo Mwalim aliyefariki ametambuliwa kwa jina la Elieza Mbwambo aliyekuwa akifundisha  darasa la tano.
Aidha pamoja na watu hao mtu mwingine aliyetambuliwa kwa jina la Focas Ntahamba pia amefariki kwa kupigwa na radi katika eneo la Bangwe mjini kigoma.
Mmoja wa walimu wa shule ya msingi ya kibirizi,WILBERT EMANUEL ambaye alikuwepo eneo la tukio amesema kuwa wamesikitishwa na tukio hilo ambalo lilitokea bila kutegemea na kuacha simanzi kubwa shuleni hapo.
Hili ni tukio la pili kutokea mkoani kigoma ambapo takriban mwezi mmoja uliopita wanafunzi    sita na mwalim wao  walikufa baada ya kupigwa na radi katika shule ya msingi nyakasanda katika kijiji cha nyachenda wilayani kasulu .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment