Image
Image

Yaya Toure asema ataendelea kuwepo Manchester City licha ya timu hiyo kufanya vibaya msimu huu


Ilitarajiwa kuwa Yaya Toure atakuwa miongoni mwa mastaa wenye majina makubwa kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu baada ya timu hiyo kuchemsha vibaya msimu huu, lakini inadaiwa kuwa staa huyo wa Ivory Coast amegoma kuuzwa.
Toure amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa ambao unampatia kitita cha Pauni 220,000 kwa wiki na staa huyo hataki kwenda katika klabu nyingine ambayo itampatia mshahara chini ya huo. Klabu nyingi kubwa Ulaya ikiwemo Inter Milan zinavutiwa na mpango wa kumchukua staa huyo lakini zinachoshwa na mshahara wake mkubwa ambao unamfanya kuwa mmoja kati ya wachezaji wanaolipwa sana Ulaya.

Inter Milan inadaiwa ipo tayari kumpa mkataba wa miaka mitano kufidia punguzo la mshahara wake wa sasa lakini haionekani kama Toure atakubali wazo hilo.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Inter Milan, Piero Ausilio hivi karibuni alikiri kwamba klabu yake bado ina ndoto za kumnyakuwa Toure ambaye aliwahi kufundishwa na kocha wao wa sasa, Roberto Mancini wakati akiwa Manchester City.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment