Akizungumza baada ya katika ofisi za Umoja wa Ulaya
mjini Brussels Mogherini amesema kila mtu ana wajibu wa kukabiliana na janga
hilo lenye kugharimu maisha ya watu. Amezitaka serikali zilizo katika Umoja wa
Ulaya kuunga mkono kwa vitendo katika jitihada za kuwalinda wahamiaji katika
Bahari ya Meditarenia.
Akikisitza wakati kuwa "wakati ni huu" wa
kushughulikia kwa haraka kwa umoja huo kukabiliana na matukio mabaya ya kufa
kwa wahamiaji, amesema wanapaswa kuokoa maisha ya wanadamu pamoja, wote kwa
pamoja wanapaswa kulinda mipaka yao sambamba na kudhibiti biashara haramu ya
binaadamu. Aidha kiongozi huyo wajuu wa Umoja wa Ulaya alisema Mawaziri wa
Umoja wa Ulaya watalijadili jambo hilo nchini Luxembourg.
Zaidi ya watu 700 wanahofiwa kufa maji baada ya bodi
iliyokuwa na msongamano mkubwa wa watu, wenye kusafrishwa kwa magendo kuzama
katika eneo la nje ya mwambao wa Libya. Tukio hilo limezusha ulazima wa Umoja
wa Ulaya kuchukua hatua ya kudhibiti mikasa ya vifo vya mauwaji hao kwa wakati
huu.
Walinzi wa ufukwe wa Italia ambao wanaratibu jitihada
za uokozi wa manusura na miili ya walokufa wanasema watu 28 tu wamefanikiwa
kuokolewa katika meli hiyo iliyozama, ambayo imeibua miito mipya kutoka kwa
kiongozi wa kanisa Katoliki dunini Papa Francis na viongozi wengine wa Umoja wa
Ulaya katika kile kinachoonekana kama mkasa unaoweza kuepukika.
Msisitzo wa UNHCR
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani UNHCR limesema
ushahidi wa walionusurika unaonesha kwamba katika boti ya uvuvi ya urefu wa
futi 70 iliyozama kulikuwemo kiasi ya watu 700.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka katika jiji la
Catania, manusura mmoja kutoka Bangladeshi ambae alipelekwa hospitali mjini
Sicily kwa kutumia helkopta anasema idadi ya waliokuwemo katika boti hiyo
inafikia watu 950 na kutaja idadi ya wanawake 200, watoto 50.
Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk
anaangaliwa uwezekano wa kufanyika mkutano mkuu maalumu wa umoja huo wakati huu
kukigubikwa na miito kutoka katika matiafa wanachama kama Ujerumani, Uhispania,
Ugiriki na Ufaransa. Katika mtandao wake wa Twitter kiongozi huyo amesema
ataendelea kuzungumza na viongozi wa Umoja wa Ulaya, Kamisheni kwa lengo la
kuondosha kabissa mikasa ya ajali.
Tukio hili la sasa lenye kuchochewa na machafuko
katika eneo la Afrika ya Kaskazini, linavunja rekodi ya lile la Malta la
Septemba 2014 ambapo watu inakadiriwa wahamiaji 500 walipoteza maisha. Na
Oktoba 2013 zaidi ya watu wengine 360 walikufa baada ya boti ndogo walikuwemo
kushika moto katika mwambao wa kisiwa cha Lampedusa. Kama tukio hili la sasa
likithibitka idadi ya watu waliokufa kwa mwaka huu wa 2015 itapundukia 1,600.
0 comments:
Post a Comment