Image
Image

Breaking News:Serikali ya Nkurunziza yapinduliwa na Jeshi nchini Burundi.


                           Meja Jenerali Godefroid Bniyombareh.
Wakati serikali ya Piere Nkuruziza ikielezwa kupinduliwa na jeshi la nchi hiyo,Rais huyo yupo hapa nchini Tanzania katika kikao cha Marais wa Jumuiya wa Afrika Mashariki, EAC jijini Dar es Salaam katika kikao cha dharura.

Katika kikao hicho Marais wa Tanzania, Kenya, Uganda,Rwanda na Burundi watajadili hali ya sintofahamu inayoendelea nchini Burundi. Kikao hicho kimeitishwa na Mwenyekiti wa sasa wa EAC,Rais Jakaya Kikwete, kwa lengo la kujadili vurugu ambazo zimekuwa zikitawala nchini Burundi.

Hata hivyo wananchi nchini Burundi wanapinga suala la Rais huyo kutaka kujiongezea muongo mwingine wa kuingoza nchi hiyo ikiwa tayari amesha kwisha kaa miongo miwili madarakani,Mahakama nchini humo pia ilimpatia kibali cha kuendelea kutangaza nia ya kugombea nchini Burundi na kuiongoza nchi hiyo.

Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi Meja Jenerali Godefroid Bniyombareh ametoa taarifa kupitia kituo cha Radio cha Isanganiro akisema serikali ya Nkurunziza imevunjwa.

Askari wamezingira kituo cha utangazaji cha serikali nchini Burudi baada ya afisa wa jeshi kutangaza kuipindua serikali ya Rais ya Piere Nkurunziza wa Burundi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment