Mwandishi wa Tambarare Halisii ameshuhudia
adha hiyo katika maeneo mbali mbali ya kata za Magaoni,Tangasisi na Mabawa
ambapo nyumba zaidi ya 100 zimezingirwa na maji yaliyokuwa na vinyesi na
kusababisha baadhi ya familia kuhifadhiwa na ndugu , jamaa na majirani kwa hofu
ya kutokea kwa magonjwa ya milipuko na kuathiri afya za wakazi wake hasa watoto
wa eneo hilo.
Baadhi ya viongozi waliokwenda kufanya
ukaguzi katika eneo hilo na kufanya mkutano wa hadhara katika soko la Magaoni,
wameiomba serikali kuingilia kati mapema kwa sababu maeneo hayo yamejengwa
taasisi za dini zikiwemo madrasa zinazokusanya idadi kubwa ya wanafunzi hali
ambayo inaweza kuhatarisha maisha yao.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la
Tanga, Bwana WINFRED LAZARO amesema halmashauri ya jiji ipo katika mkakati wa kuchimba
mfereji wa kudumu kwa ajili ya kupelekea maji hayo baharini hivyo amewaomba
wakazi walioathirika na tatizo hilo waendelee kujisitiri kwa ndugu na jamaa
hadi suluhisho la kudumu litakapopatikana.
0 comments:
Post a Comment