Shirika la Umoja wa Mataifa
la kuhudumia watoto UNICEF limesema asilimia 85 ya wakimbizi wanaoingia
Tanzania ni wanawake na watoto na tayari wamebaini 1,000 ambao wamekimbia bila
kusindikizwa na mtu wewote hivyo linamanisha changamoto wanazokumbana nazo
watoto hao ikiwamo utapiamlo.
Katika mahojiano mtaalamu wa
lishe wa UNICEF kutoka Tanzania Elisabeth Macha amesema licha ya kwamba idadi
ya waliogundulika kuwa na utapiamlo si kubwa kati ya 9000 waliopimwa hadi sasa.
Amesema vipimo na huduma
nyinginezo kwa sasa zinafanyika katika kambi ya Nyarugusu nakuongeza kuwa
usajili wa wakimbizi utakapokamilika kwa wakimbizi wengine huduma hizo
zitafanyika pia.
0 comments:
Post a Comment