Wakizungumza katika kikao cha
baraza hilo ya kujadili hoja za ukaguzi, madiwani hao wamesema pesa hizo kama
zitalipwa zitaisadia halimashauri hiyo kukamilisha miradi yake kwani ushuru wa
pamba ni moja wapo ya chanzo kikubwa cha mapato ya ndani ya halimashauri hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho,
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bwana ELASTON MBWILO amewatoa wasiwasi madiwani hao kwa
sababu serikali imeamua kuwa ushuru wa pamba uitalipwa katika halimashauri
husika na makampuni yanayonunua pamba, hivyo amewataka madiwani hao kuvuta
subira wakati serikali ikishughulikia suala hilo.
Mwaka 2014 iliamua ushuru wa
pamba ukusanywe na bodi ya pamba badla ya kulipwas katika halimashauri jambo
ambalo lilileta mtafaruku katika halimashauri nyingi hapa nchini husuani
zinazolima zao la pamba.
0 comments:
Post a Comment