Bwana SAGINI amesema hayo jijini
Mwanza wakati akifungua mafunzo kwa walimu wakuu 10,813 pamoja na maofisa elimu
wa kata zaidi ya elfu mbili za mikoa 17
ya Tanzania Bara, kuhusu kuimarisha uongozi na menejimenti za shule
kupitia kiongozi cha mwalimu mkuu pamoja na miongozo ya kukuza stadi za kusoma,
kuandika na kuhesabu.
Amesema mafunzo hayo yamekuja
wakati muafaka, kufuatia kujitokeza kwa changamoto nyingi za uendeshaji wa
shule, ikiwemo uwezo mdogo wa walimu wakuu na mafisa elimu kata kuandaa takwimu
za kielimu pamoja na kuwepo kwa walimu waliokata tamaa kutokana na walimu wakuu
na maafisa elimu kata kutotimiza wajibu wao wa kusimamia maslahi yao ipasavyo.
Mafunzo hayo yameandaliwa na
Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.>>Bonyeza
SHARE Hapo juu uwezavyo ili washkaji zako wasipitwe na Stori kama Hizi
na Tunapokea matangazo maelekezo hapo kwenye ukurasa wetu yana jieleza
kuwa wa kwanza kutangaza nasi.
0 comments:
Post a Comment