Chama cha Siasa cha APPT-Maendeleo, kimetoa tamko rasmi la kumuunga mkono mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA - EDWARD LOWASSA katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Katika taarifa yake Rais Mtendaji wa chama cha Chama cha APPT-Maendeleo, PETER KUGA MZIRAY amesema uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Mkutano Mkuu Taifa wa chama hicho, uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
MZIRAI amesema ni imani ya chama chake kwamba vyombo husika pamoja na Tume ya Taia ya Uchaguzi vitatambua kwamba kitendo hicho ni kwa mujibu wa Sheria na hivyo kitambulike rasmi.
EDWARD LOWASSA
APPT Maendeleo imesimamisha wagombea ngazi ya Ubunge na Udiwani mikoa tofauti.
APPT inaviomba vyama vyote vifanye siasa za ustaarabu ili Amani idumu nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)



0 comments:
Post a Comment