Askari wengine wawili wauawa Diyarbakir katika opesheni dhidi ya PKK.
Wanajeshi wawili wameripotiwa kuuawa katika operesheni zinazoendelea dhidi ya wapiganaji wa PKK mkoani Diyarbakir.
Maafisa wawili, Metin Aydemir na Latif Adiguzel wamepoteza maisha katika operesheni hiyo ambapo magaidi hao waliwavyatulia risase.
Taarifa zinaarifu kuwa wanajeshi watatu pia wamejeruhiwa katika shambulio hilo.
Kapika operesheni hizo, afisa Muhammet Tufan aliuawa Jumanne katika shambulio na kujeruhiwa kwa askari wengine watatu.
Operesheni dhidi ya magaidi hao wanaojaribu kuzuia barabara inayoonganisha Diyarbakir na Bingo bado inaendelea.


0 comments:
Post a Comment