Takwimu hizo zinatajwa kuwa ni kubwa ikilinganishwa na majeruhi wa ajali nyingine ambao hupokelewa kwa siku katika taasisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada
ya Kamati ya Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam kufanya ziara na
kutoa msaada katika taasisi hiyo, Ofisa Uhusiano wa MOI, Patrick
Mvungi, alisema majeruhi wengi wa ajali wanaofikishwa hapo madereva wa
pikipiki na abiria wao na watembea kwa miguu, hali inayosababisha wodi
za wagonjwa hao huzidiwa.
“Katika wodi ya Mwaisela na Sewahaji wanakolazwa majeruhi
imezidiwa, kwa mfano, katika wodi ya Mwaisela kuna wagonjwa 54 wakati
vitanda ni 33 pekee,” alisema Mvungi.
Hata hivyo,, Mvungi alisema ujenzi wa jengo jipya kwa ajili ya
majeruhi hao upo katika hatua za mwisho na litakapokamilika litakuwa na
uwezo wa kulaza wagonjwa 300.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Fadhili Mgonja, alisema
ziara hiyo ni muendelezo wa shughuli zinazofanyika katika Wiki ya
Usalama Barabarani nchini, ambayo inakwenda sambamba na maonyesho,
ukaguzi wa magari na kutoa elimu kwa wananchi juu ya usalama barabarani.
Alisema kutokana na juhudi na ushirikiano wa wadau mbalimbali,
ajali hizo zimepungua kwa zaidi ya asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka
2013 ambako kulikuwa na vifo zaidi ya 900 vilivyotokana na ajali za
barabarani.
Naye Naibu Katibu wa mabalozi wa usalama barabarani, Marlin Komba,
alisema wamekuwa wakiendelea kutoa elimu kwa jamii kutii sheria bila
shuruti ili kupunguza ajali hizo nchini.
Kumekuwapo na kasi kubwa ya ajali za bodaboda nchini na kusababisha hospitali za serikali kuzidiwa na idadi ya majeruhi.
Hali hiyo imelilazimisha Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha
Usalama barabarani kuanzisha kampeni ya kutoa elimu kwa madereva wa
bodaboda kwa kushirikiana na taasisi kadhaa kwa lengo la kupunguza ajali
hizo.Bofyakujuazaidihttp://bit.ly/1Km9TQU


0 comments:
Post a Comment