Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ametangaza mpango wake wa kuajiri maafisa 10,000 wa polisi kwa ajili ya kusaidia katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Akihutubia katika mkutano wa usalama uliofanyika mjini Abuja siku ya jumatatu, Buhari alisema kwamba serikali ya Nigeria inapanga kuajiri maafisa 10,000 wa polisi watakaopokea mafunzo maalum ya kupambana na ugaidi.
Buhari pia aliarifu kwamba usalama wa ndani ya nchi utaimarishwa kwa matumizi ya teknolojia mpya na mafunzo ya hali ya juu kwa vikosi vya polisi.
Buhari aliongezea kusema kuwa mpango wake wa kuimarisha usalama nchini Nigeria pia unajumuisha kuwekwa kwa mifumo ya kamera za CCTV katika miji mikubwa ili kurahisisha shughuli za polisi.
Nigeria ambayo ni nchi iliyokuwa na idadi ya watu milioni 175, inayo jumla ya wafanyakazi 370,000 wanaohudumu katika idara ya polisi.


0 comments:
Post a Comment