Akizungumza mjini Morogoro na wasaidizi wa
msaada wa kisheria magerezani kamishina wa sheria na
uendeshaji wa magereza dokta juma malewa amesema kwa muda mrefu mlundikano wa wafungwa na
mahabusu katika magereza ulikuwa kero kwa watuhumiwa lakini
ameshukuru shirika
la enviromental, humani rights care and gender linalosaidia
kutoa elimu ya kishria magerezani kwa kuwaelimisha wafungwa na hatimaye kuwa na
uwezo wa kujitetea kwenye mashauri mbalimbali yanayowakabili.
Mkurugenzi wa inviro care bibi loyce lema amesema ripoti za
wasaidizi wa kisheria magerezani zimebaini
katika magereza zote
nchini wamefungwa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi ambapo wameishauri
serika pamoja na taasisi za kiraia kuelekeza nguvu katika kuelimisha jamii
masuala ya ujasiliamali utakaowawezesha vijana kujiajiri na
kuongeza kipato chao hali hiyo itapunguza makosa ya uhalifu ili
kupunguza mlundikano wa wafungwa magerezani.


0 comments:
Post a Comment