Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti
wanafunzi hao akiwamo Dorice Prudence wa shule ya msingi Bilele na Lameck
Mkayu wa shule ya msingi Rumuli zote za manispaa hiyo, wamesema kuwa
wamejiandaa vizuri na wanatarajia kushinda maana walitumia muda wao mwingi
kujisomea.
Wamesema kuwa katika masomo ambayo wameanza nayo yamewapa
matumaini ya kushinda ,maana waliyofundishwa na walimu wao wameyakuta katika
mitihani yao ya kuhitimu darasa la saba.
Wanafunzi hao wametumia fursa hiyo kuwataka watoto wengine
wanaoendelea na mitihani hiyo kutulia na kufanya kwa umakini ili waweze
kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kwa manufaa ya maisha yao nay a
familia zao ya baadae.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Rumuli Damian Mwesiga
amesema kuwa walianza mitihani saa 2 asubuhi na hadi sasa hakuna tatizo lolote
liliojitoleza katika shule hiyo.
Mwesiga amesema kuwa kutokana na maandalizi waliyoyafanya
kwa wanafunzi wa shule hiyo, ana imani watafanya vizuri na kuendelea kutetea
nafasi yao ya ushindi maana katika mtihani kama huo mwaka jana, shule hiyo
ilishika nafasi ya kwanza kiwilaya.
Amesema katika shule ya msingi Rumuli ina wanafunzi 121
wanaomaliza darasa la saba mwaka huu wakiwamo wa kiume 56 na wa kike 65.
Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bilele Petrades Iganiza
amesema kuwa watoto wanaendelea vizuri na mitihani yao maana wanajiamini,
wametulia kutokana na kuandaliwa vizuri, na wanatarajia matokeo mazuri.
Iganiza ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi wa watoto ambao
wanaendelea na masomo shuleni hapo na katika shule nyingine kujitahidi katika
kujisomea kwa bidii, ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao.
Amewataka wazazi kuwanunulia watoto wao vifaa vya shule
ikiwamao vitabu, badala ya kutegemea vitabu vya serikali tu ambavyo wakati
mwingine havitoshi, ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao.
Iganiza amesema katika shule yake ya msingi Bilele kuna
wanafunzi 47 waliofanya mtihani wao wa taifa wa kuhitimu darasa la saba,
ikiwamo wa kiume 18 na wa kike 29.
Afisa elimu wa mkoa wa Kagera, Aloyce Kamamba, amesema kuwa
wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani huo ni 35,332 wakiwamo wa kiume 16,482
na wa kike 18,850 kutoka katika shule 918 zikiwamo za serikali na binafsi
katika mkoa mzima.

0 comments:
Post a Comment