Wayne Rooney aliandikisha rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Uingereza alipofunga bao la 50 kupitia mkwaju wa penaltı dhidi ya Uswizi.
Nahodha wa Uingereza Wayne Rooney atia wavuni mkwaju wa penalti katika mechi ambayo ataikumbuka milele. Bao ya Wayne Rooney ilivunja rekodi iliyowekwa na Sir Bobby Charlton miaka 45 zilizopita.
Wayne Rooney alijitayarisha kupiga penalti katika dakika ya 84 baada ya Raheem Sterling kuchezewa visivyo katika eneo la hatari. Mashabiki kwenye uga wa Wembley walisubiria kwa hamu penalti hii ya kihistoria ambayo ingevunja rekodi ya miaka 45. Naye Wayne Rooney hakuwavunja moyo. Ulikuwa muda wa furaha na kihistoria kwa Wayne Rooney na kwa mashabiki wa soka wa Uingereza. Rooney ameweza kustahimili kashfa chungu nzima kufikia kiwango cha kuwa mfungaji bora wa Uingereza.
Kabla ya bao la kihistoria la Rooney, mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane alikuwa ameiweka mbele Uingereza alipofyatua mkwaju katika dakika ya 67 baada ya kupoka pasi safi kutoka kwa Luke Shaw. Uingereza ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2 kwa nunge.

0 comments:
Post a Comment