Image
Image

ACT-Wazalendo ya chukizwa na mwenendo CCM kuingia mikataba na wawekezaji.

Chama cha ACT-Wazalendo kimeeleza kuchukizwa na mwenendo mzima wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi  kuingia  mikataba na wawekezaji  kuwa na uwazi.
Kimesema endapo wananchi watakichagua  katika uchaguzi mkuu tarehe 25  mwezi huu, kitapitia mikataba yote ya uwekezaji na serikali zilizowekeza pamoja na kampuni zote ili kuwa wazi na ukweli badala ya mfumo uliopo ambao hautoi nafasi hata kwa wabunge kuifahamu.
Mgombea Mwenza wa Urais  wa chama hicho, HAMADI YUSUF ametoa kauli hiyo  kwenye Viwanja vya Kwaraa Mjini Babati Mkoani Manyara  wakati akikinadi chama chake cha ACT-Wazalendo kwa kuwataka wapigakura kukichagua kwa kuwa sera zake zinalenga kuleta uzalendo.
Mgombea mwenza huyo  amewataka wapigakura kuacha kukurupuka katika kuwachagua viongozi kwa kufuata mkumbo, ushabiki na utashi wa wengine ama akili ya mwingine bila ya kujipima na badala yake kutafakari kwa kina ili wasije kujuta katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment