Image
Image

Balozi Francisco Caetano Jose Madeira ateuliwa kuongoza kikosi cha kulinda usalama cha Umoja wa Afrika nchini Somalia.


Dlamini-Zuma, kiongozi wa Umoja wa Afrika amefahamisha kumteua Francisco Caetano Jose Madeira kutoka Msumbiji kuwa muakilishi maalumu wa AMISOM nchini Somalia.
Francisco Caetano Jose Madeira anachukuwa wadhifa wa balozi Maman Sidikou ambae alikuwa akiongoza AMISOM tangu mwaka 2010.
Madeira atashirikiana na serikali ya Somalia, UN, Umoja wa Ulaya, Marekani na Uingereza katika harakati za kusaka amani nchini humo.
Madeira aliwahi kuongoza idara mbali mbali Umoja Wa Afrika moja wapo katika kitengo cha kupambana na ugaidi ambapo alipambana na waasi wa Uganda kati ya mwaka 2011 na 2014.
Tangu mwaka 2006 jeshi la Somalia linashirikiana na vikosi vya Umoja wa Afrika dhidi ya kundi la wanamgambo wa al Shabaab wanaodai kutaka kuweka sheria za kiislamu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment