Image
Image

mtu mmoja kufariki baada ya kuonyesha dalili zinazokaribia za ugonjwa wa Ebola.


Wasiwasi umezuka katika mji wa Calabar, kusini mwa Nigeria baada ya mtu mmoja kufariki baada ya kuonyesha dalili zinazokaribia za ugonjwa wa Ebola.
Shirika la usimamizi wa mambo ya dharura nchini humo linasema kuwa watu kumi wamewekwa karantini baada ya kugusana na mtu aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema mtu huyo alifariki punde baada ya kufikishwa hospitalini.
Sampuli za damu kwa sasa zinafanyiwa uchunguzi.
Shirika la afya duniani WHO lilitoa taarifa yake siku ya Jumatano kuwa nchi tatu zilizokuwa zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo ambazo ni Guinea, Sierra Leone na Liberia, zimefanikiwa kukaa wiki moja bila kuwa na tukio lolote la ugonjwa wa Ebola kwa mara ya kwanza kabisa tangu kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo mwezi Machi mwaka 2014.
Zaidi ya watu 11,000 walifariki dunia kwa ugonjwa huo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment