Image
Image

Vijana wametakiwa kutokubali kutumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa.

Vijana wametakiwa kutokubali kutumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa  kwa maslahi ya watu wachache huku hao wanaowatumia wanasonga mbele katika maendeleo na wao wanazidi kurudi nyuma.
Rai hiyo imetolewa na Mke wa Rais,  Mama SALMA KIKWETE alipozungumza  kwa nyakati tofauti na wananchi wa  kijiji cha Kikomolela kilichopo  jimbo la Mchinga na mtaa wa Likotwa,  Jimbo la Lindi mjini waliohudhuria kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na urais kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Mama KIKWETE ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi  kupitia wilaya ya Lindi Mjini amesema kuna baadhi ya wanasiasa wanawatumia vijana kufanya vurugu ambazo hazina faida katika jamii  zaidi ya kuleta hasara kwani wanaharibu miundombinu ikiwa ni pamoja na barabara, majengo na hivyo kurudisha maendeleo nyuma.
Kuhusu uchaguzi aliwaomba wananchi wote wa maeneo hayo wakiwemo wanachama wa  vyama vya upinzani kuwachagua wagombea wa Chama cha Mapindui  ambao watazidi  kuwaletea maendeleo kwani Serikali ya CCM imefanya mambo mengi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za afya, elimu, maji na barabara.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment