Image
Image

WFP yalenga kutoa misaada ya vyakula kwa wananchi 850,000 wa Zimbabwe wanaokabiliwa na baa la njaa.


Shrikila la Misaada ya Vyakula Duniani WFP, limetangaza mpango wake wa kutoa misaada ya vyakula kwa wananchi 850,000 wanaokumbwa na baa la njaa nchini Zimbabwe.
Uhaba wa mvua,ukame wa maji na hali mbaya ya hewa iliokuwepo katika misimu ya miaka 2014-2015, imeathiri vibaya sekta ya kilimo nchini Zimbabwe na kupunguza mavuno ya vyakula.
Kiwango cha mazao ya mahindi kimepungua kwa asilimia 40 katika mwaka wa 2015 nchini Zimbabwe na kuilazimu serikali kununua tani 700,000 za mahindi kutoka nje.
Kulingana na takwimu zilizotolewa na kamati ya utafiti, kuna takriban wananchi milioni 1.5 wanaoishi katika vijiji vya Zimbabwe wanaokabiliwa na baa la njaa.
WFP imetangaza kwamba itatoa misaada ya vyakula na kuchangia fedha dola milioni 18.5 kwa ajili ya kukabiliana na baa la njaa nchini Zimbabwe.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment