Image
Image

NEC: Waliopenya majina yao katika viti maalumu hawa hapa.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ametangaza majina ya vyama vilivyokidhi vigezo kikatiba na kisheria angalau kupata asilimia 5% katika uteuzi wa wabunge viti maalum.
Lubuva amesema katika uteuzi huo CCM viti 64,Chadema Viti 36,CUF Viti 10.
Amesema kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 66(1)(b) na ibara ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa kwa pamoja na kifungu cha kutangaza viti Maalumu vya wabunge wanawake visivyopungua asilimia 30 ya wabunge wote.
Pia amesema kuwa kwa mujibu wa uamuzi wa Serikali wa Mwaka 2010 idadi ya wabunge wanawake wa viti maalumu iliongezwa na kufikia asilimia 40,ambapo kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015 Viti maalum ni 113 (Miamoja kumi na tatu).
Hata hivyo amebainisha kuwa kutokana na kuwepo majimbo 8 ambayo hayakufanya uchaguzi basi mgawanyo wa Viti Maalum kwa sasa itakuwa 110.
Lubuva ameongeza kwa kusema kuwa katika mchakato huo viti 3 vilivyo baki vitagawanywa baada ya kufanyika kwa uchaguzi katika majimbo hayo.
Aidha amesema kuwa majina ya wabunge wa viti maalum yatapatikana katika vyama husika kwa mujibu wa orodha iliyowashwa tume na kila chama ili tume hiyo iweze kufanya uteuzi.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment