Image
Image

Ukwaju ni tiba kwa wanawake wakati wa hedhi au wakati wa tendo la ndoa.


Ukwaju ni tunda linalotokana na mkwaju, mkwaju ni mti unaotoa matunda ambayo yanajulikana kama ukwaju ambayo wengi huyatumia kwa kula au kutengenezea juisi.
Tabibu Abdallah Mandai yeye ni mtaalam wa tiba asili hapa nchini kutoka kituo cha Mandai Herbalist Clinic yeye anasema mti wa ukwaju unafaida kuanzia mizizi, magome, majani, na hata matunda yake pia,
“Tukianza na mizizi ya mkwaju ikitengenezwa vizuri huwa na uwezo wa kutibu magonjwa mengi likiwemo tatizo la mkojo mchafu (UTI)” alisema Tabibu Mandai
Aidha, tabibu Mandai anabainisha kuwa mizizi husaidia sana kuzibua mirija ya uzazi,lakini pia humpunguzia mwanamke maumivu wakati wa hedha au wakati wa tendo la ndoa.
Tabibu Mandai, anafafanua kuwa majani ya mkwaju yanapoandaliwa vizuri husaidia sana kuzuia homa za mara kwa mara ukiwemo ugonjwa wa malaria,kuharisha damu,homa ya matumbo pamoja na vidonda vya tumbo.
Hali kadhalika, majani ya mkwaju yanapokaushwa kivulini kisha kupondwa na unga wake ukichanganywa na mafuta ya nazi husaidia kuondoa magonjwa ya ngozi na muwasho.
Kwa wenye matatizo ya miguu kufa ganzi au kuwaka moto wachanganye unga wa majani ya ukwaju na mafuta ya nazi kisha mgonjwa achue eneo husika maumivu yanaondoka kabisa,”alisema Tabibu Mandai.
Mbali na faida hizo, lakini pia unga huo wa majani ya ukwaju husaidia sana kwa wale wenye matatizo ya pumu (athama), ambapo mgonjwa anapaswa kuchanganya unga huo pamoja na asali kisha mgonjwa anatakiwa alambe kwa kufanya hivyo husaidia sana kuondokana na hali hiyo pamoja na kifua kikavu.
Sambamba na hayo, Tabibu Mandai anasema kwamba “ nashauri kuwa mtu atumia juisi ya ukwaju daima angalau anywe mara mbili au hata tatu kwa siku . Kwanza inaongeza vitamin A, B na C, lakini pia ina madini ya chuma, ‘calcium’ na ‘zink’. Pia kwa wale wenye shida ya kupata choo au tumbo kuunguruma ni vizuri wakatumia juisi hiyo itawasaidia kuondokana na matatizo hayo."
Hata hivyo ni vyema ukawasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai ili kufahamu zaidi matumizi ya tiba hii. Mpigie simu Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment