Image
Image

Askari wanaokiuka haki za binadamu na maadili kuchukuliwa hatua kali za kisheria.


Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa nchini Dk.Hussen Mwinyi amesema jeshi hilo limeanza kuchukua hatua stahiki za kijeshi dhidi ya askari ambao wamekua wakienda kinyume na sheria,mila na desturi za jeshi katika kipindi chote tangu jeshi  lianzishwe mwaka 1964.
Waziri ameyasema hayo dodoma wakati akijibu swali la mbunge viti maalum Mh.Maryam Msabaha aliyetaka ufafanuzi  kuhusu hatua za kinidhamu zinazochukuliwa kwa askari wanaokiuka haki za binadamu na kwenda kinyume na sheria katika utendaji wao wa kazi hasa kutumia nguvu nyingi kwa wananchi.
Dk .Mwinyi amesema jeshi limekua likichukua hatua stahiki za kijeshi dhidi ya wakosaji kwa mujibu wa taratibu zake na wengine kupelekwa mahakamani za kiraia kulingana na aina ya kosa alilotenda muhusika na kwa wale waliokutwa na hatia walipewa adhabu stahiki kulingana na uzito w a makosa waliotenda ikiwa ni pamoja na vifungo vilivyoambatana na kufukuzwa utumishi jeshini
Ameongeza kwa kusema  kuwa ni vigumu  kubainisha  idadi  ya  askari  hao  tangu jeshi  lianzishwe  ambapo  kimsingi jeshi limekuwa likichukua  hatua stahiki za kijeshi dhidi ya wakosaji kwa mujibu  wa taratibu  zake na wengine  kupelekwa katika mahakama za kiria  kulingana  n aina ya kosa alilotenda mhusika

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment