Image
Image

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete yafanya upasuaji mkubwa wa moyo bila kuusimamisha moyo .

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete –JKCI- kwa kushirikiana na Hospitali ya BLK kutoka nchini India  kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (Buypass  Surgury )  bila kuusimamisha moyo kwa kutumia mashine maalum inayoitwa Heart Lung Machine.
Upasuaji huo  ni mkubwa  wa kwanza na wa aina yake kufanyika hapa nchini na kwa kanda Afrika ya Mashariki na Kati .
Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam  , Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dk. Peter Kisenge amesema  wataalam wa taasisi hizo mbili kwa mara ya tatu wameweza kutoa tiba kubwa ya moyo  bila mgonjwa kupasuliwa kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa kuzibua Valvu zilizoziba( BMV Procedure ).
Wataalam hao wa Moyo ambao watakuwa hapa nchini kwa siku mbili watatoa mafunzo kwa watoa huduma wa Taasisi ya moyo ambapo wagonjwa watakaopewa huduma hii watafikia takribani 18 .
“ Taasisi itaokoa zaidi ya Shilingi Milioni 180 kwa siku mbili kama wagonjwa hawa wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu haya haya ,  na kubwa zaidi si fedha tu bali tumeokoa  maisha ya watanzania wenzetu” amesema Dk. Kisenge.
Katika hatua nyingine, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete  imetia saini mkataba wa ushirikiano wa kutoa huduma na mafunzo na Taasisi ya BKL ya nchini India , lengo ni kuwapa mafunzo watumishi wake na kuendelea kutoa huduma ya upasuaji  wa moyo kwa kushirikiana na taasisi ya BLK .
Kwa mwaka huu peke yake JKCI imefanya procedure 471 ikiwemo upasuaji wa Moyo kwa kufungua kifua  99,  vipandikizi  78 , vizibua njia  265 na nyinginezo 29 .
Mbali na ushirikiano huu na Taasisi ya BLK , JKCI imeweza kufanikisha huduma hizi kubwa kwa kushirikiana na  taasisi nyingine marafiki zikiwemo Al-Muntada ( Saudi Arabia ) Open Heart  International ( Australia) , Save a Child’s Heart ( Israel)  na Madaktari Afrika.
Kambi kama hizi zitaendelea tena Julai, Septemba na Novemba .

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment