Image
Image

TANZIA:IFUNDA YAPATWA Na MSIBA:Ajali ya Pikipiki yapoteza uhai wa Hassan Ilumbo Tanga.

                                  Hassan Ilumbo -Enzi za Uhai wake 
                                     Mtoto wa Hassan Ilumbo aliye muacha.

Na.Semvua Msangi,Dar es Salaam.
Habari zilizonifikia hivi leo ni juu ya Moja ya Mwanafunzi na Mwanafamilia wa Ifunda Technical Secondary School kwamba amefariki dunia kwa ajali ya pikipiki jijini Tanga.
Kupitia Group la WhatsAPP la IFUNDA TECHNICAL Secondary School lenye zaidi ya wanachama 70 waliosoma Ifunda miaka hiyo,zilianza kutumwa Jumbe fupi za Maandishi zikieleza kuwa Hassan Ilumbo amefariki kwa ajali ya pikipiki jijini Tanga,simanzi huzuni ziligubika jukwaa hilo la wanafamilia wa Ifunda.
Aghalabu Haikuwa rahisi kuamini kwamba mmoja wa wanafamilia ametutoka, jambo ambalo liliendelea kuacha maswali lukuki takribani mwendo wa zaidi ya saa moja kwa baadhi bado kushikwa na bumbuazi ya kinachoelezwa juu ya kupoteza mwanafamilia wa Ifunda.
Kufariki haikuwashangaza sana kwa kuwa huko ndiko nyumbani na kila mmoja atarejea,lakini kilichoshangaza nimuda alioondoka angali bado ndoto zake hazijatimia,walitamani wanaifunda lau hata angejua nilini anawaacha bac hata awaage lakini siri ya mungu kuhusu kifo ndipo inapo pata nafasi ya kuendelea kuaminiwa kuwa akisema Yes hakuna wakusema No.
Marehemu Hassan Ilumbo Tangu yupo ifunda, hakuwahi kuwa mtu wa kununa,kuondoka kwake ghafla kumewakumbusha wanaifunda na hata waliosoma naye Arusha Technical College,ucheshi wake tu  kwani  kila mmoja wao anakumbuka hilo ambapo kwa sasa sirahisi kufutika mapema kwenye familia ya wanaifunda Arusha Technical College,waliosoma naye kwani imepoteza kiungo muhimu kwa wakati huu taifa likiamini vijana ndio nguvu kazi ya taifa na yenye kuleta maendeleo.
Wanafamilia wa Ifunda Technical Secondary School waliosoma tangu Mwaka 2003 mpaka 2016 niwenye kumbukumbu na hata ambao hawakusoma miaka hiyo wapo waliopata kufahamu lau kwa uchache uchangamfu wake.
Marehemu Ilimbo ni baba wa mtoto wa kike,inaelezwa Mwili wake umehifadhiwa hospitali ya Muhimbili kuangalia taratibu zingine za kifamilia.
Kupitia Familia ya wanaifunda ni kwamba Mipango ya Mazishi inafanyika Temeke Dar es Salaam,Maziko yanatarajiwa kufanyika kesho na hivyo Dada wa Marehemu kutoka Bukoba na kaka yake anayeishi Kibaha Mkoani Pwani Ndiye anayesubiriwa kwaajili ya Mambo Mengine.
watu wanakusanyika kunako msiba
Msiba unaarifiwa upo nyumbani kwao Temeke karibu na shule ya Madenge,Taratibu zingine Tutawafahamisha kadiri muda unavyo kwenda.
Ukiwa Mwanaifunda ukihitaji kutoa mchango wako basi waweza kunifahamisha chini hapo nikupe utaratibu wa kuungana na wanafamilia wa Ifunda ili Mchango wako ufike panapo stahili ili kumpumzisha ndugu yetu.
Mungu ilaze Roho ya Hassan Ilumbo Mahala Pema Amen.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments: