Image
Image

Wanahabari watakiwa kufichua maovu bila woga ili kujenga Tanzania mpya na yapamoja.

Wakati leo ikiwa ni kilele cha siku ya uhuru wa vyombo vya Habari duniani ambapo kwa Tanzania maadhimisho hayo yanafanyika jijini Mwanza,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye amewatoa hofu wanahabari na kuwataka kufichua maovu bila woga wa aina yeyote ili kuweza kujenga Tanzania ya Pamoja.
Kauli ya Nape inakuja wakati wadau wa habari sambamba na watu mbalimbali wakipaza sauti zao juu ya kutooneshwa matangazo ya Bunge LIVE kutoka Dodoma kama ilivyokuwa ikioneshwa hapo awali jambo lililopelekea hata wanahabari kutopata nafasi yakurekodi mijadala hiyo kama awali kitu ambacho kimeonesha sura tofauti ya kuzibwa mdomo kwa kile kinachotakiwa kuripoti bungeni hapo dodoma.
kuhusu sekeseke hilo Waziri nape wakati wa siku wa vyombo vya habari jijini Mwanza amesema kuwa kuhusu urushwaji wa matangazo ya Bunge LIVE bado nafasi ipo nzuri ya kukaa meza moja na wadau hao wa habari ili kuamua namna bora ya kuboresha suala hilo ili yapatikane maamuzi ya pamoja ya urushwaji wa Matangazo ya bunge kama ilivyokuwa mwanzo mwa mabunge yaliyopita.
Amesema pia kufanikisha hili watazingatia kama serikali kwamba watakapo wasilisha Sheria ya Muswaada wa vyombo vya habari Bungeni kwaajili ya kujadiliwa watahakikisha kuwa unafuta sheria kandamizi ya kama ya mwaka 1976, na hivyo kutungwa sheria mpya yenye kuzingatia sera iliyopo ambayo italingana na maoni ya wadau wa habari juu ya maboresho ya muswaada huo wa vyombo vya habari.
"Nawahakikishieni kwamba Tunatunga sheria kwa ajili ya watu Kuna sheria zinalalamikiwa kuwa na mapungufu Serikali itakaa chini kuangalia namna ya kuzirekebisha!.
Waziri Nape amewahakikishia wanahabari kwamba kama Serikali watahakikisha kuwa wanalinda,kutetea,na kuukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari Tanzania.
Aidha ameongeza kuwa uamuzi wa kuanzishwa studio ya Bunge ni uamuzi uliopitishwa na Bunge lililopita kabla hata hajawa mbunge hivyo suala hili nilenye kukaa meza moja na kufikia lengo lenye tija katika sekta hii ya habari na kila mmoja kupata habari kwa wakati.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment