Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na Watu imetoa uamuzi wa mashauri manne yaliyowasilishwa na wananchi wa mataifa ya Tanzania , Rwanda , Bukinafaso na Libya, likiwemo la mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, hayati MUAMMAR GADDAFI na mwanasiasa wa Rwanda VICTORE INGABIRE.
Shauri la raia wa Tanzania, MOHAMED ABUBAKAR linahusiana na kesi ya ujambazi wa kutumia silaha ambalo mahakama imetupilia mbali malalamiko yake baada ya kujiridhisha kwamba hakukuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa upande wa raia wa Rwanda VICTORE INGABIRE, mahakama imeeleza ana haki ya kusikilizwa na kwamba hatua Rwanda kujiondoa kwenye kipengele cha kuwaruhusu wananchi na asasi za kiraia kupeleka kesi kwenye mahakama hiyo haiwezi kuzuia shauri hilo kusikilizwa na mahakamam hiyo ya Afrika .
Kuhusu raia wa Bukinafaso ambeye ni Mwandishi wa Habari, ISSA KONETE, mahakama imeitaka serikali ya nchi hiyo kumlipa fidi, a baada ya kubaini kuwa haki zake zilikiukwa wakati kusikiliza shauri lake.
Kuhusu mtoto wa aliyekuwa rais wa Libya,SEIF GADAFFI ambaye analalamikia kukiukwa kwa haki zake, mahakama imeitaka Serikali ya Libya kuzifanyia marekebisho baadhi ya sheria zinazokiuka haki za binadamu na watu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment