Image
Image

MR.Blue aweka bayana sababu za kutumia dawa zakulevya*Pia azungumzia Mboga saba.

Mwanamuziki wa Bongo Flava Mr.Blue ameweka wazi kuwa hakuwahi kutumia Dawa za kulevya Kama unga ila alishatumia Bangi pekee tofauti na ilivyokuwa ikielezwa na baadhi ya watu na haswa kupitia mitandao ya kijamii.
Baada ya kushuka kimuziki kwa muda kidogo Mr.Blue amesema kuwa kwa sasa amekwisha kuwa mtu mzima na anafamilia hivyo haoni sababu za kuendelea na dawa hizo za kulevya(Bangi).
Unajua unapokuwa na ule umri(Fulsh,age)Kuna mambo mengi ambayo mtu unakuwa unafanya siwezi kurudia kufanya vitu vile,nawaahidi mashabiki wangu kuwa sasahivi watapata Blue ambaye ana akili timamu"Amesema Blue.
Blue amesema hayo wakati wa Mahojiano yake na Kipindi cha THE BASE na kuwa kwa zaidi ya miaka miwili ambayo alifanya kwa kutumia dawa hizo za kulevya(Bangi) maskani na yeye, sasa yupo sawa katika muziki na hajashuka kimuziki anafanya poa tu.
Katika hatua nyingine Blue ameweka wazi ukaribu wake na Ali Kiba na kusema Alikiba kwake nizaidi ya ndugu wametoka mbali mnoo,amekuwa mtu wa mwanzo kumpeleka studio kurekodi wimbo wake wa kwanza wa sinderera baada ya kutambua kuwa anauwezo, hivyo washkaji wengine wamekutana ukubwani tu.
Ali Kiba ndiye aliyeandika wimbo wa Abby Skills wa Maria naliaa, baada Abby Skills kuniletea huo wimbo ndipo nikatambua uwezo wa Kiba kwenye muziki nikampeleka studio.
Full Interview ipo Hapa tuachie Maoni yako.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment