Image
Image

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Brussels kujadili.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Brussels, kujadili mikakati ya kuepusha wanachama wengine wa Umoja huo kufuata mfano wa Uingereza, ambayo Alhamis iliyopita ilipiga kura kuondoa uanachama wake.
Mkuu wa Benki Kuu ya Ulaya, Mario Draghi, anahudhuria mkutano huo.
Maafisa wa Ulaya wanasema wanapanga mkakati wa kuzuia mkwamo wa kiuchumi na kisiasa kufuatia uamuzi wa wapiga kura wa Uingereza kuiondoa nchi yao katika Umoja wa Ulaya.
Ujerumani, Ufaransa na Italia hapo jana zilikubaliana kuwa hakutakuwa na mazungumzo yoyote kuhusu mahusiano kati yao na Uingereza, kabla nchi hiyo haijawasilisha rasmi ombi la kujiondoa katika Umoja wa Ulaya. Rais wa Ufaransa Francois Hollande alisisitiza kuwa hawana muda wa kupoteza.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, akizungumza bungeni jana alikuwa na msimamo tofauti, akisisitiza kuwa kabla ya kuwasilisha ombi hilo, Uingereza itataka kujua bayana aina ya uhusiano wa baadaye kati yake na Umoja wa Ulaya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment