Image
Image

Hillary Clinton sasa rasmi kuwania urais wa Marekani.

Wajumbe wa chama cha Democratic nchini Marekani wamemuidhinisha Bi Hillary Clinton kuwa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu.  Bi Clinton anakuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Marekani kuwa mgombea urais wa chama kikubwa cha kisiasa nchini humo.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika mjini Philadelphia aliyekuwa mpinzani wake wakati wa kura za mchujo Seneta Bernie Sanders alitangaza kumuunga mkono Bi Clinton kuwa mgombea rasmi wa chama hicho.  Mume wa Hilary Clinton, Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton naye pia alipata nafasi ya kutoa hotuba na kumuunga mkono Bi Clinton akisema kwa sasa ana sifa zinazomuwezesha kuwa rais ajaye wa taifa hilo.  Bi Clinton ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani anatarajiwa kuchuana na mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika uchaguzi huo wa Novemba.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment