Image
Image

Medeama yaibugiza Yanga bao 3-1 Kombe la Shirikisho Afrika.

Klabu ya Yanga ya Dar es salaam Tanzania imejiweka katika mazingira magumu zaidi ya kufuzu kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kuchapwa bao 3-1 na Medeama ya Ghana.
Mechi hii ni ya marudiano ambapo katika mchezo wa kwanza kati ya Yanga na Medeama uliopigwa katika dimba la Taifa Dar es salaam, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.
Kwa matokeo haya, Yanga inabaki na pointi yake 1 katika Kundi A, huku Medeama wakifikisha pointi 5 sawa na MO Bejaia, huku TP Mazembe ikongoza kwa kuwa na pointi 7.
TP Mazemba na MO Bejaia wanakutana leo nchini DRC.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment