Image
Image

9 wauawa katika shambulizi dhidi ya Chuo Kikuu cha Marekani.

Kwa uchache watu tisa waliuawa katika shambulio dhidi ya Chuo Kikuu cha Marekani katika mji wa Kabul, nchini Afghanistanje, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan.
"Wanafunzi 7 waliuawa na wengine 30 pamoja na walimu wamejeruhiwa" katika shambulizi dhidi ya Chuo Kikuu cha Marekani katika mji wa kabul Jumatano usiku, Sediq Sediqqi, msemaji wa Wizara ya mambo ya Ndani ameliambia shirika la habri la AFP, akiongeza kuwa polisi wawili pia waliuawa.
Wakati huo huo polisi imefahamisha kwamba operesheni ya kuwasaka washambuliaji imemalizika Alhamisi hii alfajiri baada ya washambuliaji wawili kuuawa, masaa kumi baada ya kuanza kwa operesheni hiyo.
"Tumemaliza kazi yetu. Washambuliaji wawili wameuawa.," Fraidoun Obaidi, mkuu wa polisi mjini Kabul ameliambia shirika la habari la AFP.
Hakuna kundi lililodai mpaka sasa kuhusika na shambulizi, ambalo linakuja wiki mbili baada ya walimu wawili wa chuo kikuu, mmoja kutoka Australia na mwengine raia wa Marekani kutekwa nyara.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment