Image
Image

Dully:Inde imenifungulia ukurasa mpya wa Music Nchini Tanzania.

Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva,Dully Sykies amefunguka na kusema kuwa wimbo wake mpya wa Inde aliomshirikisha Harmonize ni kama umemfungulia ukarasa mpya kimuziki na kujua ni aina gani ya muziki mashabiki wake walikuwa wakiutarajia kutoka kwake.
kwa upande mwingine Dully amejitapa kuwa jicho lake liliona vyema kumshirikisha harmonize kwenye wimbo huo kwani kumeongeza impact ya kazi hiyo ambayo video yake imefikisha views laki nane ndani ya wiki moja.
Kwangu mimi ‘Inde’ ni ukurasa mpya katika maisha yangu ya muziki, ni muda mrefu sijatoa ngoma ambayo imefanya vizuri kwa muda mfupi kama hii, kwa hiyo naweza kusema nimejifunza vingi, nimegundua mashabiki wa muziki wangu walikuwa wanamtaka Dully wa zamani, Dully wa kipindi kile,” alisema Dully Sykes.
Aliongeza, “Pia wazo la kumshirikisha Harmonize limeboresha sana hii kazi, nashukuru Mungu jicho langu lilikuwa zuri, mtu kama Harmonize ni msanii wa mbali sana, kwa hiyo mashabiki wategemee vitu vizuri sana kutoka kwangu
Source: Bongo 5
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment