Image
Image

Idadi ya waliofariki kutokana na Tetemeko la ardhi wafikia 250 Italia.

Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi katikati mwa Italia mapema Jumatano imefika 250,ambapo awali ilielezwa kuwa walifariki 73, huku manusura waliosalia wanaendelea kutafutwa.
Maafisa wa uokoaji wanaendelea na juhudi za kutafuta manusura na miili kwenye vifusi.
Tetemeko hilo la nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter liliharibu vibaya miji ya Amatrice, Accumoli na Pescara del Tronto ambapo watu wengi walifariki.
Maafisa wa uokoaji waliendelea na juhudi za kuwatafuta manusura usiku, lakini wakati mmoja walitatizwa na mitetemeko mingine iliyotokea na kutikisa majumba yaliyosalia yakiwa bado wima.
Eneo lililokumbwa na tetemeko hilo ni milimani katika majimbo ya Umbria, Lazio na Marche.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa karibu na Norcia, kilomita 170 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Roma.
Mahema yamewekwa kuwasaidia watu walioachwa bila makao.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment