Image
Image

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.2 laua watu 73 Italia.

Watu takriban 73 wamefariki baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter maeneo yenye milima katikati mwa Italia.
Watu wengine wengi wamefukiwa chini ya vifusi.
Wengi wamefafiki katika kijiji cha Pescara del Tronto ambacho kimeharibiwa vibaya na inahofiwa kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na sita usiku saa za Italia (01:36 GMT), 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa Perugia, katika kina cha 10km (maili sita) chini ya ardhi, taasisi ya Marekani inayohusika na mitetemeko ya ardhi USGS imesema.
Mitetemeko ilisikika katika miji ya mbali kama vile Roma, Venice, Bologna na Naples. Mjini Roma, baadhi ya majumba yalitikisika kwa sekunde 20, kwa mujibu wa gazeti la La Repubblica.
Mji wa Amatrice nao pia uliharibiwa vibaya. Watu wanne wanahofiwa kufariki katika mji jirani wa Accumoli.
Eneo hilo, ambalo linapatikana katikati mwa mikoa ya Umbria, Lazio na Marche, ni maarufu sana kwa watalii na kuna wageni wengi waliokuwa eneo hilo kipindi hiki cha shughuli nyingi za kitalii.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa Norcia, karibu na Perugia.
Tetemeko hilo awali lilikisiwa kuwa la ukubwa wa 6.4. Lilifuatwa na mitetemeko mingine mikubwa, gazeti la Repubblica limeripoti.
USGS wamesema uharibifu huenda ukawa mkubwa.
Mwaka 2009, tetemeko la ardhi la nguvu ya 6.3 lilitokea eneo la Aquila, na kusikika pia katika mji wa Roma. Watu zaidi ya 300 walifariki.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment