Image
Image

Maambukizi ya UKIMWI tishio, Bara la Afrika linaongoza.

Ugonjwa wa UKIMWI unasalia kuwa janga duniani hasa kwa mataifa mbalimbali ya Afrika.
Takwimu kutoka Shirika la afya duniani WHO zinaonesha kuwa asilimia 69 ya watu Kusini mwa jangwa la sahara, wanaishi na virusi vya HIV.
Watu walioambukizwa barani Afrika ni Milioni 25.8.
Maambukizi hayo sio makubwa sana Kaskazini mwa Afrika ikilinganishwa na hali iliyo hasa katika Mataifa ya Kusini mwa bara Afrika.
Asilimia 10 ya watu kutoka nchi za Bostwana, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Naimibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbawe wameathiriwa.
Madaktari na wanasayansi nchini Afrika Kusini wamekuwa wakifanya vipimo kuona ikiwa watafanikiwa kupata chanjo ya UKIMWI.
Namna mtu anavyoambukizwa HIV
  • Njia kubwa ni kushiriki ngono na mtu aliyeathirika.
  • Kuchangia vifaa vyenye ncha kali kama sindano na mtu aliyeathirika.
  • Kuongezewa damu kutoka kwa mtu aliyeathirika kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
  • Kutoka kwa mama aliyeathirika hadi kwa mtoto wakati wa kujifungua.
Sababu za maambukizi kuongezeka.
1. Tabia-Utafiti uliofanywa na mashirika mbalimbali kama WHO barani Afrika, unaonesha kuwa watu wanaojihusisha katika ngono na zaidi ya mpenzi mmoja, wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi.
2.Hali ngumu za kiuchumi- Kutokana na ugumu wa maisha, wanawake wengi hasa wasichana huamua kujiuza ili kujipatia kipato. Mfano nchini Kenya, madereva wa malori yanayosafirisha mizigo wameendelea kukabiliana na hali hii.
3.Kutahiri na kukeketa-
Kutahiri kwa wanaume na kukeketwa kwa wanawake kwa njia ya kitamaduni hasa barani Afrika nchini Kenya, Lesotho na Tanzania kumeendelea kuhatarisha maisha ya wengi.

Takwimu muhimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa UNAIDS
  • Watu Milioni 36.7 wanaishi na virusi vya ukimwi duniani.
  • Watu wengine Milioni 17.1 walioambukizwa hawafahamu ikiwa wameambukizwa.
  • Maambukizi mapya kila mwaka ni karibu Milioni 1.9 kufikia mwaka 2015.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment