Image
Image

Kimbunga chaua 18 kusini mwa Marekani, wengine wajeruhiwa.



Watu zaidi ya 18 wamefariki kutokana na kimbunga kikali na hali mbaya ya hewa kusini mwa Marekani, maafisa wa uokoaji wamesema.
Watu wengi wamejeruhiwa Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni majimbo ya Georgia na Mississippi.
Gavana wa Nathan Deal ametangaza hali ya tahadhari katika wilaya saba kusini na katikati mwa Georgia ambapo watu 14 wamefariki.
Watu wanne waliuawa na vimbunga Mississippi siku ya Jumamosi.
Bado kuna hatari ya kimbunga kupiga maeneo ya kusini mwa Florida, idara ya taifa ya hali ya hewa imeonya.
Idara ya huduma za dharura ya Georgia imesema watu 14 walifariki katika wilaya za Cook, Brooks, Dougherty na Berrien katika jimbo la Georgia.
Nyumba nyingi zimebomolewa katika wilaya ya Cook.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema amewasiliana na Gavana Deal na kumpa salamu za rambirambi kutokana na vifo vilivyotokea.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment