Image
Image

Viongozi wa Afrika kukutana Addis Ababa ethiopia, kumchagua mwenyekiti mpya wa umoja huo.

Viongozi wa mataifa ya Afrika, watakutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia mwishoni mwa wiki hii kujadili maswala mbalimbali yanayoligusa bara la Afrika hususan kuhusu usalama na uchumi.
Hata hivyo, viongozi hao watakuwa na kazi kubwa ya kumchagua Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja huo kuchukua nafasi ya Nkosazana Dlamini-Zuma(Pichani Hapo)kutoka Afrika Kusini.
Wagombea watano wanawania wadhifa huu akiwemo Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Bi Amina Mohammed.
Serikali ya Kenya inasema ina imani kubwa kuwa mgombea wake atashinda, kwa mujibu wa Waziri wa Elimu Fred Matiang'i ambaye amekuwa akiongoza Kamati Maluum ya kumpigia debe Waziri Amina(Pichani hapo).
Itafahamika kwamba Afrika Mashariki itawakilishwa na Fowsiyo Yusuf Haji Adan, waziri wa zamani wa kigeni nchini Somalia, na Waziri wa sasa wa mambo ya Nje wa Kenya Amina Mohammed, ambaye anapigiwa debe na Rais wake, Uhuru Kenyatta, na kuungwa mkono na rais wa Uganda Yoweri Museveni. Moussa Faki Mahamat, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, ambaye alitangaza kuwania katika kinyang'anyiro hicho katika dakika ya mwisho, ni miongoni mwa wagombea hao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment