Image
Image

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin amefariki.



Churkin, ambaye angetimiza miaka 65 Jumanne, alifariki ghafla akiwa kazini mjini New York Jumatatu, wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilisema kupitia taarifa.
Chanzo cha kifo cha mwanabalozi huyo hakijabainika.
Bw Churkin amehudumu kama balozi wa Urusi katika UN tangu 2006 ambapo alijizolea sifa kama mtetezi wa dhati wa sera za Urusi.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema alisikitishwa snaa na kifo cha mwanamume huyo ambaye kipaji chake cha uanadiplomasia kilienziwa sana.
Runinga ya taifa Rossiya24 ilimsifu kwa kuwazidi nguvu wapinzani wake na mara nyingi kuwaacha wakiwa "hawana la kusema".
Wengi wa "wapinzani" hao wamekuwa pia wakituma salamu za rambirambi kwa mwenzao huyo wanayesema kwamba ingawa hawakukubaliana naye sana, walimheshimu sana.
Balozi wa Uingereza Matthew Rycroft ameandika kwenye Twitter kwamba amehuzunika sana kusikia habari za kifo cha Churkin naye Gerard Araud, balozi wa zamani wa Ufaransa wa UN akikumbuka ustadi na ucheshi wa Churkin.
Balozi wa Marekani Nikki Haley amesema alikuwa mtu mwema kufanya kazi naye, na kuongeza kwamba: "Ingawa hatukutazama mambo kwa njia sawa, alitetea msimamo wa taifa lake kwa ustadi mkubwa".
Mtangulizi wa Haley, Samantha Power, pia ameeleza kusikitishwa kwake na kifo cha Churkin kwenye Twitter.
Bw Churkin, alizaliwa Moscow, na alikuwa mwigizaji alipokuwa kijana ambapo aliigiza katika filamu mbili kuhusu Vladimir Lenin.
Baadaye, alijiunga na taasisi ya mambo ya nje ya Moscow na baadaye akaanza kazi kama mwanabalozi katika wizara ya mambo ya nje ya Urusi.

Kabla ya kuanza kazi UN, alihudumu kama balozi Canada, Ubelgiji na kama mwakilishi maalum katika mazungumzo kuhusu uliokuwa muungano wa Yugoslavia miaka ya 1990.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment