Image
Image

RC Ruvuma atoa siku 7 kuvunjwa nyumba ya kulala wageni iliyojengwa kwenye chanzo cha maji.

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Dk Binilith Mahenge ametoa siku saba kwa Idara ya Mipango Miji ya Manispaa ya Songea mkoani hapa kuvunja nyumba ya biashara katika mtaa wa Miembeni ya mkazi wa eneo hilo, Iman Mbugi iliyojengwa ndani ya mita 20 kutoka chanzo cha maji.
Agizo hilo limekuja baada ya malalamiko ya muda mrefu ya wakazi wa mtaa huo kwamba mfanyabiashara huyo kwa kutumia uwezo wake wa fedha amejenga nyumba ya kulala wageni katika eneo hilo ambalo ni jirani na chanzo cha maji na kusababisha wananchi wengine kukosa maji.
Alitao agizo hilo wakati wa kikao chake na wenyeviti wa mitaa katika manispaa ya Songea kilichofanyika Ikulu Ndogo, mjini hapa.
Aidha, amewaonya baadhi ya watumishi wa idara hiyo na idara ya ardhi katika manispaa hiyo kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria badala ya kutanguliza tamaa ya fedha kutoka kwa matajiri ambao wamekuwa wakisababisha migogoro mingi na hata wanawadhulumu wanyonge maeneo yao.
“Nawapa siku saba kuhakikisha kwamba hiyo nyumba inavunjwa, kama mtaalamu wa mazingira amejiridhisha kwamba iko ndani ya meta 20 kutoka chanzo cha maji ni vema mkatekeleza wajibu wenu,” alisema Dk Mahenge.
Kwa mujibu wake, maofisa wa mipango miji hawapaswi kuogopa kutekeleza agizo lake, kwani kuna sheria ambayo inayopiga marufuku kufanyika kwa shughuli zozote kwenye vyanzo vya maji.
Dk Mahenge amewataka wenyeviti wa mitaa kusimamia sheria ndogo ndogo za uhifadhi mazingira na vyanzo vya maji na kutoogopa kusimamia sheria hizo, kwani ni wajibu wao wa kila siku kuhakikisha sheria zilizopo zinasimamiwa na kutekelezwa.
Awali, Mwenyekiti wa mtaa huo, Christian Komba alimweleza mkuu wa mkoa kwamba katika mtaa wake kuna mfanyabiashara amejenga nyumba katika chanzo cha maji na kusababisha watu wengine kukosa huduma hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment