Image
Image

Uchaguzi TLS kufanyika, kesi ya kupinga uchaguzi huo yatupiliwa mbali na Mahakama kuu.

Ile kesi ya kupinga uchaguzi wa TLS iliyofunguliwa Dar es Salaam na Dodoma imetupiliwa mbali.
Kesi moja ilifunguliwa Mahakama Kuu, Dar es Salaam na wakili Onesmo Mpinzile. Wakili Masha na wenzie amewahenyesha waliofungua kesi hiyo mpaka wakaishiwa pumzi na leo rasmi jaji kaitupilia mbali.
Kesi ya Dodoma ambayo wakili Wasonga alipigwa mapingamizi kumi na tano ya kisheria na kikosi cha wanasheria visiki wakiongozwa na Lissu nayo imetupiliwa mbali na mahakama imemtaka Wasonga kulipa gharama za kesi.
Wakili Wasonga alitaka kuiondoa kesi hiyo baada ya kuona "misumari" ya kisheria ya akina Lissu lakini akina Lissu waligoma,wakataka wasikilizwe ili wamchape kweli kweli,hakika walimchapa wakili huyo wa CCM na maamuzi ni Leo.
Mapingamizi hayo yaliibomoa kesi hiyo na kila kitu kilitupwa na ilibaki paragraph moja tu ,jina la mahakama na mleta maombi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment