Image
Image

Waziri Mwakyembe aguswa na kifo cha Mchora Nembo ya Taifa Mzee Ngosha

Dar es Salaam. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya msanii mkongwe katika fani ya uchoraji Mzee Francis Maige Kanyasu (86), aliyefariki usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Habari, imeeleza kuwa Waziri Mwakyembe amemwelekeza Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa, Godfrey Mngereza, kushirikiana kwa karibu na ndugu na jamaa wa marehemu katika mazishi yake.
“Wizara itahakikisha michango ya wasanii wakongwe kama Mzee Kanyasu, inafuatiliwa kwa karibu na kuwekewa kumbukumbu kwa faida ya vizazi vijavyo.” imesema taarifa hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment