Image
Image

Waziri Ummy Mwalimu: Tanzania haijafikiwa na ugonjwa wa Ebola.

"Kupitia wataalam wa afya waliopo katika mipaka ya nchi serikali itakuwa ikitoa taarifa za mara kwa mara ya namna uzuiaji wa ugonjwa huo kwa wananchi na wanapata elimu ya kutosha ya kujikinga na virusi vya Ebola", alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy aliongeza kuwa wananchi wanashauriwa kutoa taarifa pamoja na kupata elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola kwa kupiga simu namba 117 na kupata huduma bila ya malipo kwa mitandao yote.
Aliongeza kuwa Serikali imeendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu wake walioko mipakani ikiwa ni pamoja na utoaji wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo pamoja na vidonge kwa wataalamu hao walioko mipakani.
"Serikali tayari imeagiza mashine nne kwa ajili ya kufanya vipimo katika mipaka yetu pamoja na viwanja vya ndege na bandari zetu na tutahakikisha kila mgeni anayewasili nchini kutokea Congo anasajiliwa," alisema Waziri Ummy.
Ugonjwa wa Ebola unasababishwa na kugusa majimaji yanayotoka kwa mgonjwa mwenye virusi vya Ebola na mizoga na dalili za ugonjwa huu zinatokea baada ya siku mbili pindi mgonjwa anapopata maambukizi ya ugonjwa huo zikiwemo kutokwa na damu sehemu za puani, masikioni na homa kali.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment