Image
Image

Madereva 24 wa malori kutoka Tanzania watekwa na waasi wa Maimai Congo.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano  imeliomba Jeshi  la Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Congo linalopambana na kikundi cha waasi cha Maimai  kuwa makini  katika mapambano yao  ili kunusuru maisha ya  madereva 24 wa  malori  kutoka Tanzania waliotekwa nchini humo kwa hofu ya  kutumika  kama ngao ya mapigano baina yao.
Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki imebaini jitihada mbalimbali zilizokwisha chukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa ikiwemo kukutana na Waziri wa mambo ya ndani na ulinzi na mkuu wa kikosi cha MONUSCO ili kuona namna ya kuwalinda na kuwarudisha nyumbani madereva hao ambao wameendelea kukwama nchini humo licha ya kuachiwa huru kwa hofu ya usalama wao wakiwa njiani.
Makamu Mwenyekiti TATOA Bwana Elias Lukumai licha ya kupongeza jitihada zinazoendelea kunusuru madereva hao wameiomba serikali kuweka ubalozi mdogo katika eneo la Lugumbashi nchini DRC utakaorahisisha mawasiliano kwa kutambua hali ya usalama nchini humo.
Baadhi ya madereva walionusurika kutekwa nchini humu wameelezea hali ya usalama kuwa mbaya na kutoa wito kwa serikali kuharakisha jitihada za kuwarudisha nyumbani madereva wenzao.
Madereva 24,21 kati yao wakiwa ni watanzania walitekwa na kikundi cha waasi cha Maimai terehe 29 Juni mwaka huu katika eneo la Lulimba kilimota mia moja kutoka jimbo la Kivu ya Kusini na kuachiwa huru kwa shari la kuacha magari yao.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment